Polisi Tanzania yamnasa mwanajeshi wa Marekani akiwa na mabomu manne 

November 17, 2025 11:36 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Polisi yasema inaendelea kukusanya ushahidi na kumhoji mtuhumiwa.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi nchini limesema limemkamata Charles Onkuri Ongeta, mwenye uraia pacha wa Marekani na Kenya na cheo cha Sajenti katika Jeshi la Marekani, akidaiwa kuingia nchini akiwa na mabomu manne ya kurushwa kwa mkono aina ya CS M68.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Mark Njera tukio hilo limetokea Novemba 16, 2025 majira ya saa 6:00 mchana katika eneo la mpaka la Sirari, wakati mtuhumiwa akijaribu kuingia Tanzania akitokea Kenya kwa kutumia gari aina ya Toyota Landcruiser.

Kwa mujibu wa Njera, silaha hizo ni marufuku kuingizwa nchini kwa mujibu wa sheria za Tanzania.

“Kwa mujibu wa sheria ya umiliki wa silaha, mabomu ya aina hii hayaruhusiwi kabisa kuingizwa nchini. Hata kama angeomba kibali, asingeruhusiwa kuyapitisha,” amefafanua

Jeshi la Polisi limesema, linaendelea kukusanya ushahidi na kumhoji mtuhumiwa kuhusu tuhuma hizo, kabla ya kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks