Tumia zana hizi kuthibitisha habari zilizotengenezwa na akili bandia
- Zana hizo ni pamoja na ‘FotoForensics’ na ‘Fake Image Detector’.
Arusha. Matumizi ya akili bandia yanaendelea kushika kasi maeneo mbalimbali duniani yakiwasadia waatumiaji kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo za kitaaluma au kiofisi.
Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia (WB) hadi kufikia Machi 2024 karibu watu bilioni 3 walitumia programu za akili bandia ikiwemo Chat GPT.
Programu hizo huunda maudhui kwa rangi na ubunifu wa hali ya juu zaidi ya uwezo wa binadamu suala linaloweza kuchochea kuongezeka kwa ta habari za uzushi au uchochezi katika majukwaa ya kidigitali.
Kwa mujibu wa tovuti ya NewsGuard, ambayo hufuatilia tovuti za habari za uongo, mwaka 2023 idadi ya tovuti zinazotumia AI kusambaza habari feki iliongezeka mara kumi ukilinganisha na miaka mingine.

Wakati maudhui yanayotengenezwa na AI yakiongezeka, zipo zana mbalimbali zinazoweza kukusaidia kuthibitisha habari, picha aua video iliyotengenezwa na akili bandia.
Miongoni mwa zana hizo ni FotoForensics ambayo huchambua picha ili kubaini kama zimebadilishwa kwa kutafuta alama za upungufu wa faili unaotokea wakati picha inapohaririwa na kuonesha maeneo yenye mashaka.
Mbinu nyingine ni ‘Fake Image Ditector’ ni zana inayobaini picha zilizohaririwa kwa kutumia mbinu za kisasa kama uchambuzi wa taarifa binafsi na uchambuzi wa makosa (Error Level Analysis).
Mbali na hiyo ipo Sensity AI inayootumia akili bandia kuchambua miondoko ya uso na sauti ili kubaini picha na video feki pamoja na zana ya AI or Not ambayo husaidia kutambua kama picha ni ya kweli au imetengenezwa kwa kutumia akili bandia.
Latest



