SAU na ndoto ya kumaliza tatizo la ajira nchini
- Yasema itamaliza tatizo hilo kupitia sekta ya kilimo, viwanda na teknolojia.
Arusha. Chama cha Sauti ya Umma (SAU), kimezindua kampeni zake kwa nafasi ya urasi, ubunge na udiwani huku kikiahidi kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini ikiwa kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi kwa miaka mitano ijayo.
Mgombea Urais wa wa Tanzania kupitia Chama cha SAU, Majalio Kyara aliyekuwa akizungumza na katika uzinduzi wa kampeni hizo Ukonga, Dar es Salaam leo Septemba 9, 2025 amesema chama hicho kitatengeneza mfumo utakaotambua vipaji vya vijana ili kupambana ukosefu wa ajira.
“Vijana wengi wanakosa ajira kwasababu hakuna mfumo sahihi wa kuwezakutambua vipaji vya vijana wetu sisi kama SAU tunataka kutengeneza mfumo madhubuti ukaoweza kutambua vipaji vya vijana wetu…
… Mfumo huo utambue vipaji uvilee, uvikuze ili viweze kusaidia katika mandeleo ya mtu mmoja mmoja ya Taifa letu.
Mgombea huyo ametoa ahadi hiyo wakati ambapo idadi ya wahitimu wa shule na vyuo inaongezeka kila mwaka huku nchini Tanzania huku nafasi za ajira zikiwa chache jambo linaloongeza idadi ya vijana wasio na ajira Tanzania.

Mgombea Urais wa wa Tanzania kupitia Chama cha SAU, Majalio Kyara akiwasili katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho.Picha?TBC online
Kyara amebainisha kuwa chama hicho kina vipaumbele vitatu ambavyo ni kilimo, viwanda na teknolojia ambavyo vyote vikitumiwa vyema vinaweza kumaliza kabisa tatizo hilo la ajira.
“Kupitia kilimo tunakwenda kutatua changamoto nyingi kwenye Taifa letu ikiwemo afya, ajira na mambo mengine mengi hata uchumi wa Taifa na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.
Kwa upande wake mgombea mweza wa nafasi ya urais kupitia chama hicho Satia Bebwa amewataka wananchi waliohudhuria kampeni hizo kupiga kura za ndio kwa chama hicho kwa wingi ili waweze kutekeleza ahadi mbalimbali ikiwemo kutoa elimu bure, uzazi bure kwa wajawazito na pembejeo kwa wakulima.
“Hatutaki mzaha kwa sasa hivi tunataka kufanya kazi ajili yenu. Tupeni kura muone tutakachokifanya, hatutakaa mjini tutakaa pembezoni mwa mji ili tujue matatizo yenu,” amesema Bebwa