INEC yakamilisha uteuzi wagombea urais, ACT, ADC wawekwa kando
- Ni kutokana na madai ya ukiukwaji wa taratibu za kisheria katika mchakato wa uteuzi ndani ya vyama vyao.
Arusha. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekamilisha vimekalisha zoezi la uteuzi wa wagombea wa kiti cha rais na makamu wa rais kwa vyama vya siasa 16 huku wagombea wawili wa vya vya ACT Wazalendo na Alliance For Democratic Change (ADC) wakiwekwa kando.
Uamuzi huo wa INEC umefikiwa mara baada ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutengua uteuzi wa Luhaga Mpina wa ACT-Wazalendo na Wilson Elias wa ADC, kwa madai ya ukiukwaji wa taratibu za kisheria katika mchakato wa uteuzi ndani ya vyama vyao.
Zoezi hilo la uteuzi limefanyika leo Agosti 27, 2025 katika ofisi za INEC jiji Dodoma kuanzia saa 2;00 asubuhi hadi saa 10:00 alasiri likisimamiwa na Jaji Jacobs Mwambegele ambaye ni mwenyekiti wa tume hiyo pamoja na wajumbe wengine.
Chama cha Mapinduzi (CCM) ndiyo kilikuwa chama cha kwanza kuwasili katika ofisi hizo ambapo wagombea walioteuliwa ni Rais Samia Suluhu Hassan na Dk Emmanuel Nchimbi ambaye ni mgombea mwenza.
Baada ya kuwasili katika ofisi hizo, Jaji Mwambagele amesema kuwa wagomea hao wa CCM wamekidhi vigezo kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.
Wagombea waliopendekezwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi hii ya kiti cha rais na makamu wa rais wametimiza masharti ya ibara ya 39 ndogo ya kwanza ibara 41 na ibada ya 47 ndogo ya nne ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mwaka 1997 ikisomwa pamoja na kifungu cha 34 cha Sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sheria namba. 1 ya mwaka 2024,”amesema Jaji Mwambagele.
Vyama vingine vilivyofika katika ofisi hizo kwa nyakati tofauti tofauti kwa ajili ya uteuzi ni pamoja na National Reconstruction Alliance (NRA) ambapo walioteuliwa ni Hassan Kisabya Almasi na Hamisi Ali Hassan, wengine ni Coaster Jimmy Kibonde na Azza Haji Suleiman wa Chama cha MAKINI,
Mbali na hivyo, INEC imevitaja vyama vingine vilivyowasili kwa ajili ya uteuzi huo ni Chama cha Wananchi (CUF), Democratic Party (DP), Union for Multiparty Democracy (UMD).
Tanzania Democratic Alliance ADA (TADEA), National League for Democracy (NLD), Sauti ya Umma (SAU), Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), NCCR Mageuzi, Chama Cha Kijamii (CCK) na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).
Baada ya kuzuiliwa kuingia ACT Wazalendo imelaani tukio hilo ikisema kuwa imekiuka na kuvunja Katiba ya Tanzania huku ikiituhumu INEC kufuata maagizo ya watawala badala ya kutenda haki.
“ Chama chetu kimefuata na kuzingatia utaratibu wote wa kisheria katika zoezi hili. Badala yake tunazuiwa kushiriki uchaguzi kwa maelekezo ya watawala. Watawala wanamuogopa Mpina. Watanzania wanapaswa kukataa haya mambo, imesema taarifa ya ACT.
Ikiwa vyama hivyo havijaridhika na uamuzi wa tume vinaruhusiwa kukata rufaa kabla ya kesho Agosti 28 saa 10: 00 jioni ambapo zoezi hilo litafungwa,
Latest



