Othman ajinadi kuwania urais Zanzibar

August 23, 2025 2:31 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema uzoefu alioupata katika kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini unampa sifa na uhalali wa kuongoza Zanzibar.
  • Aongeza kuwa Zanzibar inahitaji mageuzi makubwa ili ipate maendeleo endelevu.

Dar es Salaam. Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman amejinadi kuwania urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akiahidi mageuzi makubwa kwa maslahi ya wananchi.

Othman amesema uzoefu alioupata katika kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini unampa sifa na uhalali wa kuongoza Zanzibar kuelekea maendeleo endelevu ikiwemo kushughulikia mfumo wa utoaji haki.

“Haya ni katika mambo ya msingi na sisi tunaamini tuna majibu yake,”amesema Othman aliyekuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari leo Agosti 23, 2025 jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa ACT wazalendo othman Masoud, leo akiongoza kikao cha kamati Kuu. Picha/ ACT wazalendo.

Othman  aliyechukua fomu za kuwania nafasi hiyo kwa upande wa Zanzibar Aprili 13 mwaka huu ataungana na Luaga Mpina mgombea wa  urasi kwa tiketi ya chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara  kuomba ridhaa ya wananchi kuingia madarakani Oktoba 29 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Othman, ACT itashughulikia changamoto nyingine zilizopo nchini ikiwemo elimu, utawala bora, ajira, huduma za kijamii na uwezeshaji wananchi kiuchumi, uwezeshaji wananchi katika maisha,huduma za kijamii na matumizi ya teknolojia mambo alaiyoyatajja kuchangia mageuzi Zanzibar.

Othman amebainisha kuwa chama chake kimeamua kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 licha ya changamoto zinazotokana na mazingira ya kisiasa kuelekea uchaguzi huo.

”Lazima tukubali kwamba uchaguzi wa 2020 na maandalizi yanayofanywa kwa sasa hivi ni mabaya zaidi na huku tunapoelekea pengine kutakuwa na maafa zaidi. Leo tumefika tuna nchi ambayo busara peke yake iliyobakia ni matumizi ya nguvu,” ameeleza Othman.

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks