Simu za rununu bado zipo zipo Tanzania

February 1, 2025 11:41 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ueneaji wa vifaa hivyo umeongezeka kwa asilimia 2.8 ndani ya kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Arusha. Matumizi ya intaneti yamezidi kushika kasi nchini yakichangia kuongezeka kwa watumiaji wa simu janja zinazowawezesha kuperuzi katika mitandao ya kurasa mbalimbali.

Licha ya kukithiri kwa matumizi ya simu hizo takwimu mpya za mawasiliano zinazotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinabainisha kuwa idadi kubwa ya Watanzania bado wanatumia simu za rununu maarufu kama ‘viswaswadu’.

Takwimu hizo za robo ya mwaka unaoishia Disemba 2024 zinabainisha ueneaji wa simu za rununu umefikia asilimia 87.39 ambapo jumla ya vifaa milioni 56.8 vimeunganisha na mtandao.

Kwa mujibu wa TCRA ueneaji wa vifaa hivyo umeongezeka kwa asilimia 2.8 kutoka asilimia 84.8 iliyorekodiwa katika robo ya mwaka unaoishia Septemba 2024.

Wakati matumizi hayo ya simu za rununu yakiongezeka matumizi ya simu janja nayo yameongezeka mpaka asilimia 35.9 kutoka asilimia 33.8.

Hiyo ni sawa na kusema idadi ya vifaa vya simu janja vilivyounganishwa na mtandao hadi kufikia Disemba ni milioni 23.4.



Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks