Mauzo ya bidhaa za Tanzania nchini Marekani yapaa kwa asilimia 7

May 23, 2024 11:14 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Kwa mwaka 2023, mauzo yameongezeka hadi  Sh205.8 bilioni kutoka Sh192.26 bilioni ya mwaka 2022.
  • Bidhaa hizo ziliuzwa kupitia Mpango wa Ukuzaji Fursa za Kiuchumi Afrika (AGOA).

Dar es Salaam. Mauzo ya bidhaa za Tanzania kwenda Marekani kupitia Mpango wa Ukuzaji Fursa za Kiuchumi Afrika (AGOA) yameongezeka kwa asilimia 7 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja yakichagizwa na ongezeko la bidhaa za nguo na mavazi zinazouzwa katika soko hilo.

Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 imeeleza kuwa kwa mwaka 2023, mauzo ya bidhaa za Tanzania nchini Marekani yalikuwa Sh205.8 bilioni.

Mauzo hayo yameongezeka kutoka Sh192.26 bilioni ya mwaka 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji akiwasilisha bajeti ya wizara yake hivi karibuni, amesema kuwa ongezeko hilo limechangiwa na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa za nguo na mavazi zinazouzwa katika soko hilo. 

Mauzo ya bidhaa za Tanzania nchini Marekani katika kipindi cha miaka mitano iliyopita yamekuwa yakipanda na kushuka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo janga la Uviko-19.

Mathalan, mwaka 2019, mauzo yalikuwa Sh141.6 bilioni na yakashuka hadi Sh103.2 bilioni mwaka 2020.


Soma zaidi:Wizara ya Viwanda na Biashara imeomba kuidhinishiwa bajeti ya Sh110.9 bilioni kwa mwaka 2024-25


Mauzo hayo yalipungua zaidi hadi Sh84.6 bilioni mwaka 2021, mwaka ambao shughuli za usafirishaji wa bidhaa zilisimama katika nchi mbalimbali ikiwa ni hatua ya kujikinga na Uviko-19.

Hata hivyo, baada ya wadau wa afya kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo ikiwemo utoaji wa chanjo, mauzo yalianza kuongezeka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, na huenda yakaongezeka zaidi miaka ijayo baada ya Serikali kuimarisha mazingira ya biashara.

Hotuba ya bajeti ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka 2021/22 imeeleza kuwa katika mwaka huo wa fedha, Serikali iliandaa Mkakati wa Kitaifa wa Kukuza Mauzo ya Tanzania katika soko la Marekani kupitia mpango huo wa AGOA.

Marekani yaipiku Tanzania kwa mauzo

Wakati mauzo ya bidhaa za Tanzania nchini Marekani yakiimarika, pia mauzo ya nchi hiyo kuja Tanzania nayo yameongezeka.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa katika tovuti ya AGOA, mauzo ya bidhaa za Marekani nchini Tanzania kwa mwaka 2023 yalikuwa ni Dola za Marekani 424.9 milioni (Sh1.06 trilioni) yakiongezeka kutoka Dola za Marekani 260 milioni (Sh600.3 bilioni) za mwaka 2022.

Hilo ni sawa na ongezeko la asilimia 63.4 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Baadhi ya bidhaa zikichakatwa katika moja ya viwanda vilivyochini ya  Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA).Picha|EPZA/X(Twitter).

AGOA ni nini?

Mpango wa Ukuzaji Fursa za Kiuchumi Afrika (AGOA) ni mpango uliowekwa na Serikali ya Marekani kusaidia kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi hiyo na nchi za Afrika. 

Inatoa fursa kwa nchi za Afrika kuuza bidhaa zao kwa urahisi katika soko la Marekani bila ushuru au vikwazo vingine vikubwa vya kibiashara. 

Pia inalenga kuchochea ukuaji wa viwanda na ajira katika bara la Afrika.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wananchi kupima afya, kuacha uoga

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wananchi kupima afya, kuacha uoga

Nukta TV

Uwepo wa vifaa, madaktari uendane na huduma inayotakiwa

Uwepo wa vifaa, madaktari uendane na huduma inayotakiwa

Nukta TV

Rais Samia: Maradhi ya moyo, saratani kwa watoto yaongezeka Tanzania

Rais Samia: Maradhi ya moyo, saratani kwa watoto yaongezeka Tanzania

Nukta TV