Google yadaiwa fidia ya mabilioni kwa kutumia mashairi ya nyimbo bila taratibu

December 5, 2019 10:06 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Inadaiwa kwamba Google wamekuwa wakitumia nyimbo kutoka Genius kwenye kitafutishi chake bila kufuata taratibu.
  • Hii ni mara ya pili mwaka huu Google kuingia matatani baada ya kupewa barua ya onyo kutoka Genius.
  • Septemba 2019 Tume ya Shirikisho la Biashara ya Marekani (FTC) waliitoza Google faini ya dola za Marekani milioni 170. 

Dar es Salaam.  Kampuni ya Marekani ya Genius inayohusika na kutoa mashairi ya nyimbo mbalimbali (Lyrics) za muziki wa Hiphop na Rnb imeomba fidia ya  Dola za Marekani milioni 50 (Sh115 bilioni) kampuni ya Google baada ya mtandao huo kutumia baadhi ya mashairi yake bila kufuata taratibu.

Genius wanadai kuwa Google wamefanya makosa ya kutumia mashairi yake katika kitafutishi chake cha Google (Google Search) bila kufuata taratibu za kisheria zinzohitajika licha ya kupewa onyo Aprili mwaka huu.

Shauri la madai hayo linaloihusisha Google na mshirika wake LyricFind, lilifunguliwa Desemba 3 mwaka huu katika moja ya mahakama Brooklyn, Newyork nchini Marekani. 

Tovuti ya habari za teknolojia ya the Verge inaeleza kuwa Genius wamebaini nyimbo nyingi zinapotafutwa kwenye kitafutishi cha Google zinatoka kwa kampuni hiyo ya Genius.


Zinazohusiana:


Moja ya mbinu zilizotumika na Genius kubaini makosa hayo ni kwa kuwa na alama (Watermark) zilizowasaidia kujua nyimbo zilizokuwa zikitumika na mtandao wa Google kutoka kwenye nyimbo zao.

Pia, taarifa hiyo imeeleza kuwa kitendo hicho hakiendi tu kinyume na taratibu za kampuni hiyo, bali wanapata faida zisizokuwa za halali kwa miaka 10 mfululizo.

Hata hivyo, hili sio sakata la kwanza lililoipata kampuni hiyo. Septemba 2019 Tume ya Shirikisho la Biashara ya Marekani (FTC) iliitoza faini ya Dola za Marekani milioni 170 sawa na Sh390 bilioni kampuni ya Google baada ya mtandao wake wa Youtube kukiuka sheria ya faragha kwa watoto (Child privacy).

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV