Chama ushirika Nyanza chatakiwa kuandaa mikakati ya kujitegemea

April 30, 2020 5:11 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akingea na watumishi wa Bodi ya Pamba nchini ambapo amewataka kubuni mikakati mipya ya kuongeza uzalishaji wa pamba nchini ili kukidhi mahitaji ya viwanda vya kuongeza thamani ya zao hilo.Tukio hili limefanyika leo jijini Mwanza. Picha| Wizara ya Kilimo.


  • Ni baada ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo kutokuridhishwa na utendaji wa chama hicho cha ushirika.
  • Ameagiza mali za chama hicho ambazo zinamilikiwa bila uhalali ziandikishwe kuwa mali za umma.
  • Pia, kiongozi huyo ameagiza bodi ya pamba kuongeza uzalishaji wa zao hilo hadi tani zaidi ya 500000 kwa mwaka ujao.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya imekiagiza Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Mwanza (Nyanza) kubuni njia muafaka za kujitegemea kiundeshaji kwa kutumia rasilimali nyingi ilizonazo.

Kusaya amesema wizara yake ina lengo la kuiona Nyanza inasimama yenyewe, kuwa ya kisasa na ikijiendesha kibiashara na kuboresha maisha ya wakulima wa mikoa inayolima zao la pamba. 

“Tunataka kuona sasa Nyanza mnakuwa na utendaji unaolenga kujiendesha kibiashara tofauti na ilivyokuwa zamani ili wakulima wa pamba wanufaike na ushirika  kupitia mali zao” amesema Kusaya leo (Aprili 30, 2020) wakati alipofanya kikao na watumishi wa chama hicho na kueleza juu ya kutoridhishwa na hali ya utendaji wa chama hicho.

Kiongozi huyo ameagiza chama hicho kipeleke ripoti yake wizarani ifikapo Mei 15 mwaka huu kwani kina mali nyingi zikiwemo nyumba, maghala na mashamba ambayo kwa sasa hayatumiki kuzalisha mali kwa faida na kuwa mali zingine bado zinamilikwa bila uhalali na baadhi ya watu.

“Watieni moyo wana ushirika ili wawe na imani na Nyanza.Nataka nione mkijitegemea na kuwa leo nilitegemea kusikia ripoti ya mafanikio badala ya kunieleza matatizo ya madeni,” amesema.


Soma zaidi: Wakulima kuuza pamba kwa bei wanayoitaka


Aidha, kiongozi huyo amegusia agizo Waziri Mkuu kuhusu urejeshwaji wa nyumba nane zilizokuwa zikimilikiwa isivyo na watu binafsi litekelezwe kwa nyumba hizo kuwa na hati miliki za umma.

Kaimu Meneja Mkuu wa Nyanza Martha Ndeto amesema tayari nyumba saba zilizokuwa zikimilikiwa kinyume ya utaratibu zimerejeshwa na hati zake zipo kwa Msajili wa Ardhi na kuwa kazi ya kuifuatilia nyumba moja iliyobaki inaendelea.

Ndeto ametaja changamoto zinazokikumba chama hicho kuwa ni pamoja na madeni ambayo hadi kufikia leo, yamefikia Sh4.23 bilioni kutoka kwenye benki, taasisi za Serikali na wafanyabiashara.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV