Zoom kuwaanika wahalifu mtandaoni

June 4, 2020 11:29 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Imefanya mabadiliko katika sera yake ya faragha kwa watumiaji wasiolipia huduma zake. 
  • Imesema imedhamiria kufanya kazi na vyobo vya dola ili kukomesha uhalifu ukiwemo unyanyasaji wa kingono kwa watoto na makundi mengine.
  • Imesema programu hiyo bado ni salama na ya uhakika. 

Dar es Salaam. Kwa wewe unatumia programu tumishi (App) ya Zoom kwa ajili ya mawasiliano ya video bila kulipia hautakuwa na siri tena katika mazungumzo yako baada ya kufanyika mabadiliko katika programu hiyo.

Uongozi wa kampuni ya Zoom Video Communications unaosimamia programu hiyo umeondoa faragha ya moja kwa moja (end to end encryption) baina ya watu wanaoutumia programu hiyo bila kulipia.

“End to end encryption” ni mfumo wa faragha ambao hauruhusu mawasiliano ya watu yaingiliwe na mtu wa tatu asiyehusika. 

Mitandao mingine inayotumia sera hiyo ya faragha ni pamoja na WhatsApp na Signal.

Mkurugenzi wa Zoom Eric Yuan amesema maamuzi hayo yamefikiwa kwa sababu Zoom inafanya kazi kwa karibu na vyombo vya dola ili kuzuia uhalifu ambao huenda mawasiliano yake yanafanyika kwenye mtandao huo.

“Watumiaji wasiolipia hakika hatuhitaji kuwapatia faragha hiyo kwa sababu tunahitaji kufanya kazi na vyombo vya dola endapo baadhi ya watu wanatumia Zoom kwa nia mbaya,” amesema Yuan.

Kwa sasa sera hiyo itawafaidisha wateja waliolipia huduma hiyo ya mawasiliano ya video mtandaoni ili kuwalinda dhidi uvamizi wa watu wasio na nia njema. 


Zinazohusiana


Hatua hiyo ya Zoom inakuja baada ya kuwepo malalamiko mbalimbali ikiwemo ukatili wa kijinsia na watoto unaofanyika katika mtandao huo na hivyo kuleta ugumu kwa mamlaka na vyombo vya dola kufuatilia uhalifu huo. 

Zoom imesema haifuatilii vikao vya watu na wala kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama lakini pale inapobidi hufanya hivyo. 

Maboresho  hayo yanalenga kuweka usawa na usalama kwa makundi ambayo yapo kwenye hatari wakiwemo watoto.

Hivi karibuni Idara ya Sheria nchini Marekani iliikatalia Facebook kutumia teknolojia hiyo kwenye mtandao wake.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV