Ujenzi wa bandari kuchochea uchimbaji mafuta, gesi asilia Zanzibar
- Mchakato wa kuwahamisha wananchi na upembuzi yakinifu katika eneo la Mangapwani Unguja itakapojengwa bandari hiyo umeanza.
- Kukamilika kwa bandari hiyo kutachochea shughuli na tafiti za mafuta na gesi katika maeneo ya bahari na nchi kavu.
- Awataka wananchi kuachana na taarifa za vijiwenikuhusu maendeleo ya utafutaji wa mafuta na gesi visiwani humo.
Dar es Salaam. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amesema wameanza kuhamisha wananchi katika eneo la Mangapwani Unguja itakapojengwa bandari ya mafuta na gesi asilia ikiwa ni hatua ya kuendeleza rasimali hiyo muhimu katika ukuaji wa uchumi na kuwanufaisha wananchi wa visiwa hivyo.
Novemba 2016, Rais huyo alisaini hati ya muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016 na ilipofika Octoba 2018 walisaini makubaliano na kampuni ya RAK GAS ya Ras al Khaimah ya kutekeleza mipango ya utafiti na utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika eneo la bahari na nchi kavu.
Dk Shein aliyekuwa akihutubia leo (Januari 12, 2018) uwanja wa Gombani Pemba katika maadhimisho ya miaka 55 ya Mapainduzi ya Zanzibari yaliyofanyika mwaka 164, amesema kukamilika kwa bandari hiyo kutasaidia kuchochea shughuli za uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ambayo utafiti wake unaendelea.
“Katika jitihada ya kuendeleza sekta ya mafuta na gesi asilia, serikali imeamua kujenga bandari ya mafuta na gesi asilia Mangapwani na tayari eneo hilo limeshapimwa, ujenzi wa barabara, kupeleka umeme na ujenzi wa matangi ya mafuta,” amesema.
Amesema shughuli za kuandaa eneo hilo zimeanza kutekelezwa ikiwemo kuwahamisha wananchi na kuwapeleka katika eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya mkazi yao ili kupisha mkandarasi kuanza ujenzi.
“Vilevile eneo maalum limetengwa kwajili ya ujenzi wa nyumba za wananchi ili kupisha eneo la mradi, upembuzi yakinifu wa hatua ya mwanzo umekamilika kwa ajili ya ujenzi huo,” amesema.
Zinazohusiana: Statoil yaja kivingine uchimbaji gesi Tanzania
Amebainisha kuwa sambamba na hilo utafiti mwingine wa rasimali hiyo katika eneo la maji madogo la visiwa vya Pemba umeanza na baadaye utaendelea katika maeneo mengine ya Unguja.
“Kwa mujibu wa mkataba huo, sasa kampuni ya RAK GAS imeidhinishwa rasmi kufanya kazi ya utafutaji gesi asilia katika kitalu cha Pemba Zanzibar,” amesema Dk Shein huku akiwataka wananchi wa visiwa hivyo kuwa wavumilivu na kufuatilia taarifa za Serikali kuhusu rasilimali hiyo.
Kuanza kwa uchimbaji wa mafuta na gesi asilia huenda ukawaondolea umaskini wananchi visiwa vya Zanzibar. Picha|oilandgaspeople.com
Suala la Zanzibar kuchimba mafuta na gesi asilia lilianza kuleta mvutano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar tangu mwaka 2009, huku baadhi ya wabunge wakisema suala hilo ni la Muungano na wengine wakipinga.
Mvutano huo ilimwalizwa mara baada ya bunge la Tanzania kutunga Sheria ya Mafuta namba 21 ya mwaka 2015 ambayo Agosti mwaka huo huo ilitiwa saini na Rais Kikwete kuwa sheria kamili.
Kutokana na sheria hiyo, Zanzibar ikaachiwa ajiamulie kuendeleza rasilimali za mafuta na gesi bila kuingiliwa na Serikali ya Muungano.
Akihitimisha hutuba yake leo, Dk Shein amesema Serikali ya Zanzibar itaendelea kuimarisha shughuli za biashara katika yake na Tanzania bara ikiwemo kuongeza mnyonyoro wa thamani wa biadhaa za kilimo na viwandani, ujenzi wa bandari ndogo na meli mpya za mafuta.
Pia kuimarisha shughuli za utalii wa fukwe ili kuongeza mapato yatokanayo watalii wanaokuja nchini kutembelea vivutio mbalimbali.
Hata hivyo, sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanziabar zimefanyika bila ya hazikuhudhuriwa na Rais John Magufuli ambaye amepata dharura. Viongozi wengine ambao hawakuhudhuria ni pamoja na marais wastaafu wawili Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete,