Ziara ya Rais Magufuli Ruvuma yamng’oa kigogo wa halmashauri

April 9, 2019 11:19 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Dk Oscar Mbyuzi aliyefutwa kazi na Rais Magufuli leo. Picha|Mtandao.


  • Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Dk Oscar Mbyuzi ambaye uteuzi wake umetenguliwa leo na nafasi yake imechukuliwa na Jimson Mhagama.
  • Sababu za kutenguliwa kwa Mmkurugenzi huyo bado hazijatajwa.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Dk Oscar Mbyuzi.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu leo (Aprili 9, 2019) inaeleza kuwa kufuatia uamuzi huo, Rais Magufuli amemteua Jimson Mhagama kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ambapo uteuzi wa Mhagama unaanza mara moja.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijaweka bayana sababu za kigogo huyo kutolewa katika nafasi hiyo.

Mabadiliko hayo ya uongozi yanakuja wakati Rais Magufuli akikamilisha ziara ya siku sita mkoani Ruvuma aliyoanza tangu Aprili 4 mwaka huu ambapo leo anazindua kituo cha afya cha Madaba kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.

Akiwa mkoani humo, Rais ametumia muda wake mwingi kuwaonya viongozi wa Serikali wakiwemo wakuu wa wilaya kutimiza majukumu yao kikamilifu na kuhakikisha wanawatumikia wananchi kwa kuwaondolea shida zao ikiwemo kuboresha huduma za kijamii.  

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV