Rais Kenyatta kuzuru Chato kwa mwaliko wa Magufuli

July 3, 2019 2:40 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Atawasili Ijumaa Julai 5 katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.
  • Atakutana na kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli.

Dar es Salaam. Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta anatarajia kufanya ziara binafsi ya siku mbili nchini Tanzania itakayoanza Ijumaa, Julai 5 katika Wilaya ya Chato mkoani Geita ambako atakutana na kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli ambaye yuko wilayani humo kwa ajili ya mapumziko. 

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa leo (Julai 3, 2019) inaeleza kuwa Rais Kenyatta anakuja nchini kwa mwaliko wa Rais Magufuli.

Rais Kenyatta atatua katika uwanja wa ndege wa Chato saa 4:00 asubuhi na kisha kuelekea katika makazi ya Rais Magufuli yaliyopo katika kijiji cha Mlimani katika Wilaya hiyo iliyopo Kusini Magharibi mwa Tanzania. 

Akiwa nchini, Rais Kenyatta atafanya mazungumzo na mwenyeji wake kabla ya kurejea nchini Kenya. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV