NBS kutoa taarifa ya mfumuko wa bei za bidhaa, huduma Novemba 11

November 8, 2019 9:56 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo imeahirisha kutangaza mwenendo wa mfumuko wa bei za bidhaa na huduma  kwa mwaka unaoishia Oktoba 2019 kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.
  • Badala yake itatangaza jumatatu ya Novemba 11.

Dar es Salaam. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo imeahirisha kutangaza mwenendo wa mfumuko wa bei za bidhaa na huduma  kwa mwaka unaoishia Oktoba 2019 kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake, badala yake itatangaza jumatatu ya Novemba 11.

Kawaida, NBS hutoa takwimu za mfumuko wa bei tarehe nane ya kila mwezi na imekuwa ikifanya hivyo kwa muda mrefu sasa. 

Taarifa iliyotolewa leo (Novemba 8, 2019) na Mtakwimu Mkuu wa NBS, Albina Chuwa  imeeleza kuwa kwa mwezi huu, takwimu za mfumuko wa bei hazitotolewa leo na badala yake zitatolewa Jumatatu ya Novemba 11, 2019.

“NBS inapenda kutaarifu wateja wake kuwa; toleo la taarifa ya mfumuko wa bei kwa mwezi Oktoba, 2019 zilizotakiwa kutolewa Novemba 8, 2019 zimeahirishwa hadi jumatatu ya Novemba 11, 2019 kuanzia saa 7:00 mchana,” ameeleza Chuwa katika taarifa hiyo. 


Zinazohusiana


Kwa mwezi uliopita wa Oktoba, taarifa hiyo ilitolewa kama ilivyo kawaida huku ikionyesha kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini ulishuka hadi kufikia asilimia 3.4 kwa mwaka ulioishia Septemba 2019.

Kilichochangia hayo yote ni kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula zikiwemo mafuta ya taa, petroli na majiko ya gesi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Nukta TV

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Nukta TV

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Nukta TV