Mfumo wa kielektroniki wa taarifa za usafirishaji wazinduliwa Tanzania

December 10, 2019 11:30 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Umezinduliwa na wadau wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) 
  • Utasaidia kuwapunguzia wafanyabiashara gharama za usafirishaji wa bidhaa katika nchi za jirani ikiwemo Zambia.

Dar es Salaam. Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imezindua mfumo wa kielektroniki wa habari za manunuzi, uuzaji  na usafirishaji (NFLIP) utakaowasaidia wafanyabiashara kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa katika nchi za jirani ikiwemo Zambia. 

Mfumo huo umezinduliwa leo (Desemba 10, 2019) jijini Dar es Salaam na Jukwaa la Wafanyabiashara Tanzania kwa kushirikiana  na wadau kutoka TPSF utakaotumika katika nchini na nchi jirani.

Akizindua mfumo huo, Mwenyekiti wa Kampuni ya Simba Group, Azim Dewji amesema kuwa, mfumo huo utawarahisishia wafanyabiashara kwa kupunguza gharama za usafirishaji kutoka eneo moja kwenda jingine.

“Mfumo huu utasaidia sana,badala ya mtu kutoka hapa kwenda Zambia au Congo kununua mzigo, ukifika kule, utatafute hoteli, utatumia usafiri wa ndani ya nchi uliopo, mawasiliano ya ndani hiyo ni gharama, lakini ukitumia mtandao wa NFLIP utaokoa gharama nyingi kwani utafanya hayo yote kwa wakati mmoja,”, amesema Dewji.


Zinazohusiana: 


Mfumo huo unamuwezesha mfanyabiashara kupata taarifa mbalimbali zinazohusu bidhaa na huduma zinazotolewa nchini na nchi jirani, jambo linaloweza kumsaidia kufanya maamuzi sahihi ya muda na pesa wakati anasafirisha bidhaa hizo

Akizungumza na wanahabari mara baada ya uzinduzi wa mfumo huo, Mkurugenzi wa Miradi ya Uendelezaji wa Biashara kutoka TPSF, Edward Furaha amesema teknolojia hiyo itaongeza ufanisi kwa wafanyabiashara kwa kupunguza gharama na muda unaotumika katika usafirishaji wa bidhaa.

’Mfumo huu unawahusu wafanyabiashara, wasafirishaji na wenye bidhaa, hivyo ni teknolojia itakayowaweka pamoja watu wote hao kwa wakati mmoja na kwa gharama nafuu,” amesema Furaha. 

TPSF imekuwa mdau muhimu katika kuboresha mazingira ya sekta binafsi nchini ikiwemo kutumia mifumo ya kidijitali yenye tija kwa wafanyabiashara na Serikali. 

/
No matches found for this filter
31 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV