Will Smith kutikisa kumbi za sinema kwa filamu ya “Spies in Disguise”

December 27, 2019 5:19 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

Spies in Disguise imemuunganisha Smith na nguli wengine kwenye tasnia ya sauti za katuni na filamu wakiwemo Karen Gillan aliyeshiriki pia filamu za “Jumani”, “Guardian of the Galaxies” na “Avangers End Game” ambapo katika filamu hiyo ameigiza sauti ya “Eyes”. Picha|Mtandao.


  • Inamhusisha muigizaji nguli Will Smith wa Marekani.
  • Imegaharimu takriban Sh11 bilioni ikiongozwa na Nick Bruno.
  • Itakufundisha kushirikiana na wale usiowatarajia wakiwemo maadui katika maisha yako. 

Dar es Salaam. Baada ya kuogelea siku ya Krismasi na kutembelea sehemu zingine za burudani, hakika wewe na watoto wako mnastahili kupata sehemu mtakapo “Relax” na kufurahia kiyoyozi na mfuko wa bisi.

Kufanya hivyo, kwanini usichague kumbi za kuangalizia filamu za Century Cinemax? Kama una mpango huo, tembelea Aura Mall, Mlimani City na maduka mengine makubwa (Malls) kama Mkuki House na Dar Free Market (DFM) ya jijini Dar es Salaam.

Ni nini kipya?

Baada ya kumbi hizo kurindima kwa filamu za “Star Wars”, “Jumanji” na “Frozen II”, msanii wa Marekani na hapo awali mwanamuziki wa miondoko ya Hiphop, Will Smith anafunga mwaka na filamu ya katuni ya “Spies in Disguise”,  hatua inayokamilisha ushiriki wake kwenye filamu tatu kwa mwaka 2019.

Baada ya ya kushirikia katika filamu za “Alladin” na “Gemini Man”, Smith (Lance Sterling) anageuka njiwa mpelelezi anayemtegemea mwanasayansi Walter Beckett japokuwa wawili hao ni maji na mafuta.

Licha ya kwamba safari yao ni ndefu kwa kuwa bado wanahitaji kujifunza kufanya kazi pamoja, inawalazimu kutegemeana kwani bila kufanya hivyo usalama wa dunia upo karibu kutoweka.


Zinazohusiana:


Hakika unahitaji kufuatilia filamu hii iliyogharimu mpunga wa takriban Sh11 bilioni huku ikiongozwa na Nick Bruno ambaye alifurahisha wapenda filamu za katuni kupitia filamu za Rio, Ice Age na Epic.

Spies in Disguise imemuunganisha Smith na nguli wengine kwenye tasnia ya sauti za katuni na filamu wakiwemo Karen Gillan aliyeshiriki pia filamu za “Jumani”, “Guardian of the Galaxies” na “Avangers End Game” ambapo katika filamu hiyo ameigiza sauti ya “Eyes”. 

Mbali na Karen, yupo Rachel Brosnahan aliyeigiza sauti ya Wendy Beckett pamoja na Tom Holland ambaye ni kichwa nyuma ya filamu ya “Spider Man”. Unakosaje kuwaona mastaa hawa?

Kwa gharama ya Sh10,000 kwa siku zingine zote kasoro Alhamisi (Sh5000), unaweza kufurahia filamu hii iliyojaa mafunzo ya kutegemeana na kufanya kazi kwa ushirika yaani “team work”.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV