Hizi ndizo shule zilizoshika mkia matokeo ya kidato cha nne 2019

January 24, 2020 8:02 am · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Shule tatu  kati ya 10 zinatoka Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  • Zanzibar imeingiza shule saba kati ya 10  katika shule zilizofanya vibaya.
  • Shule ya Kijini imeingia katika orodha hiyo kwa mara pili mfululizo.

Dar es Salaam. Kwa mara nyingine tena shule za Zanzibar zimeshindwa kujinasua katika orodha ya shule 10 za mwisho kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2019, baada ya kuingiza shule saba katika orodha hiyo. 

Orodha hiyo ya matokeo inayopatikana katika tovuti ya Necta inaonyesha shule hizo 10 zilizofanya vibaya zaidi katika matokeo hayo ya mwaka jana ni pamoja na Mgogoni iliyopo Mkoa wa Kaskazani Pemba ,Wagero (Mara), Songa (Tanga), Matemwe (Kaskazani Unguja), Uzi (Kusini Unguja) na Makoongwe (Kusini Pemba).

Nyingine ni Kinyasini iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja, Msuka (Kaskazini Pemba), Kijini (Kaskazini Unguja) na Kipoke ya Mbeya ambayo imekuwa ya mwisho kitaifa.


Zinazohusiana.


Kipoke imeporomoka kutoka nafasi ya 737 iliyoshika mwaka 2018 hadi nafasi ya mwisho kitaifa kati ya shule 3,908 zilizoshiriki mtihani huo mwaka jana.   

Kwa mujibu wa takwimu hizo za Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) Mkoa wa Kaskazini Unguja ndiyo umeingiza shule tatu ukifuatiwa na Kaskazini Pemba ambao umeingiza shule mbili huku mikoa iliyobaki ikiingiza shule moja moja. 

Shule ya Wagero kutoka imeporomoka kutoka nafasi ya 833 mwaka 2018 hadi 3900 mwaka jana ikiwa ni zaidi ya  mara nne. 

Shule ya Sekondari ya Kijini ndiyo shule pekee iliyoingia tena katika orodha ya shule 10 za mwisho kama ilivyokuwa mwaka 2018 huku shule tisa zikiingia kwa mara ya kwanza.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.