Thamani ya mauzo ya sato, kambale yapaa

January 30, 2020 12:14 pm · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Thamani ya uzalishaji wa samaki wa maji baridi aina ya sato na Kambale umeongezeka mara tano kutoka Sh21 bilioni mwaka 2014  hadi Sh111bilioni mwaka 2018.
  • Mwaka 2018, uzalishaji wa samaki hao uliongezeka hadi kufikia tani 14,800 ikilinganishwa na tani 11,000 zilizozalishwa mwaka 2017.

Dar es salaam. Thamani ya uzalishaji wa samaki wa maji baridi aina ya sato na Kambale umeongezeka mara tano kutoka Sh21 bilioni mwaka 2014  hadi Sh111bilioni mwaka 2018, jambo linalosaidia kutunisha mfuko wa mapato ya Serikali. 

Kitabu cha hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2018  kinaeleza kuwa tangu mwaka 2014 uzalishaji wa samaki aina ya sato na kambale umekuwa ukiongezeka kila mwaka na kuongeza mapato yatokanayo na votoweo hivyo. 

Mathalani, Mwaka 2018, uzalishaji wa samaki (sato na kambale) uliongezeka hadi kufikia tani 14,800 zenye thamani ya Sh111 bilioni ikilinganishwa na tani 11,000 zilizozalishwa mwaka 2017.

Thamani ya samaki hao waliozalishwa mwaka 2018 ni mara tano zaidi ya wale waliozalishwa mwaka 2014, jambo linalofungua fursa kwa wavuvi na Serikali kufaidika na mapato yanayopatikana.

Mapato hayo yamekuwa yakitumika kuboresha maisha katika kaya na kuchangia katika ukuaji wa pato la Taifa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV