Bei ya viazi mviringo yaibua tofauti Lindi, Njombe

April 1, 2020 11:11 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei inayotumika leo Lindi ni mara nne zaidi ya Njombe, jambo linalowafaidisha zaidi wafanyabiashara ambao wamepeleka viazi mviringo mkoani humo. 
  • Gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya mkoani Lindi  linauzwa kwa Sh120,000, wakati masoko ya Njombe linauzwa kwa Sh30,000.

Dar es Salaam. Watumiaji wa viazi mviringo hasa kutengeneza chipsi katika Mkoa wa Lindi na mji wa Mpanda katika Mkoa wa Katavi leo watalala na maumivu kutokana na bei ya jumla ya zao hilo kuuzwa mara nne zaidi ya bei inayotumika katika Mkoa wa Njombe. 

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa na WIzara ya Viwanda na Biashara  leo (Machi 20, 2020) zinaeleza kuwa gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya Mpanda na Lindi  linauzwa kwa Sh120,000, wakati masoko ya Njombe linauzwa kwa Sh30,000.

Hiyo ina maana kuwa bei inayotumika leo Mpanda na Lindi ni mara nne zaidi ya Njombe, jambo linalowafaidisha zaidi wafanyabiashara ambao wamepeleka viazi mviringo mkoani humo. 

Bei hiyo inayotumika Lindi ndiyo bei ya juu huku ya Njombe ikiwa ni ya chini ikilinganishwa na bei zinazotumika katika maeneo mengine nchini.

Viazi mviringo ni miongoni mwa mazao makuu ya chakula ambavyo vimekuwa vikutumiwa kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kukaanga chispi ambazo zinapendwa zaidi na mabachela. 

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW