“The Old Guard”: Jeshi la watu watano dhidi ya dunia

June 26, 2020 10:13 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu inayohusu mashujaa walio na uwezo wa kupona majeraha yoyote.
  • Wanapoibuka watu wanaohitaji vinasaba (DNA) vyao wanajikuta katika mtego wa kumaliza maisha yao.
  • Katika filamu hiyo utashudia mapambano yasiyo na kifani.

Dar es Salaam. Kundi la watu wanne ambao ni mashujaa wanajikuta katika hatari baada watu kuanza kuwafuatilia ili kuchambua vinasaba vyao.

Ni baada ya watu hao kufahamu kuwa mashujaa hao wana nguvu ya kupona majereha yoyote wanayopata na hivyo kuwa na uwezo wa kutokufariki dunia.  

Nani asiyetaka kuishi milele? Tena bila maumivu ya muda mrefu?

Baada ya wanne hao wakiongozwa na Andy (Charlize Theron) kufahamu kuwa ni panya wanaosubiriwa kunasa kwenye mtego wa paka, wanaanza kupigania maisha yao.

Loo! Kumbe yupo mwingine mwenye nguvukama wao na hawamfahamu. Baada ya kumfahamu, inabidi wamlinde kwa kuwa hafahamu ni nini kipo ndani yake.

“Tumeilinda dunia hii tukipigana katika vivuli. Ni kama haiwezekani kabisa kutoweka katika dunia tunayoishi kwa sasa,” anasema Andy akimwambia binti Nile Freeman (Kiki Layne).

“Wanaenda kutufungia na kutujaza na silaha. Lakini hawajawahi kukutana na jeshi kama letu” Andy anamsisitizia Freeman.


Zinazohusiana


“Jeshi la watu wa tano? Hebu tuanzishe bendi,” anatania Freeman.

Kama umezoea kuwaona wanawake kujipamba kwa mapambo na kufurahia maisha, unahitaji kubadilisha mtazamo wako kwa kumtazama Andy ndani ya filamu ya “The Old Guard”.

Humo yupo na Booker (Matthias Schoenaerts), Joe (Marwan Kenzari), na Nicky (Luca Marinelli) huku wakiwindwa na kiongozi Copley (Chiwetel Ejiofor).

Watakamatika? Nguvu zao zitawasaidia? Na Freeman, ataweza kuendana na kasi ya wenzie? 

Shuhudia mapanga, risasi na silaha zisizo na majina kwa kutazama filamu hii kwenye Neftlix ifikapo Julai 10.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV