Usidanganywe! Apple haigawi simu za iPhone bure
- Kampuni hiyo ya Marekani imezushiwa kuwa inagawa bure simu aina ya iPhone kwa wanafunzi na wafanyakazi.
- Habari hiyo ni uzushi kwa sababu Apple haijatangaza kutekeleza zoezi hilo wakati huu wa Corona.
Dar es Salaam. Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao wamekutana na taarifa mtandaoni inayosema kuwa kampuni ya Apple inagawa bure simu za iPhone na umeiamini, basi fahamu umedanganywa. Kampuni hiyo haijatoa tangazo kama hilo na ni habari ya uzushi yenye lengo la kupotosha.
Taarifa hiyo inasambaa hasa katika akaunti ya Facebook ya Iphone Giveaway 2020. Ilichapishwa Julai 4, 2020 kwa lugha ya Kiingereza kuwa, “IPHONE LATEST GIVEAWAY FOR STUDENTS AND WORKERS IPHONE company is ready to give away 10,000 brand new phones to people because of this pandemic period.
FREE IPHONE PHONES FOR STUDENTS & WORKERS TO WIN IPHONE Comment a lot of “I” to have a big chance to win!! and to be noticed by us in the comment section No Scammer Please Let’s Help!! ❤️❤️ Then Come inbox! via “SEND MESSAGE” button bellow With the Screenshot of your comment.”
Kwa tafsiri isiyo rasmi taarifa hiyo inaeleza kuwa “iPhone ipo tayari kutoa simu mpya za iPhone 10,000 kwa wanafunzi na wafanyakazi katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Kupata simu za bure za Iphone kwa wanafunzi na wafanyakazi. unatakiwa kutoa maoni sio utapeli. Tafadhali tusaidiane! Kwa hiyo nitumie maseji ukiambatanisha na picha ya ujumbe wa maoni yako.
Zinazohusiana
- Utapigwa: Hakuna mabilioni ya msaada wa corona yanatolewa na akaunti ya Facebook
- Corona yachangia wanafunzi 4,000 kupata mimba Kenya
Ukweli ni upi?
Habari hizo za ugawaji wa simu za Iphone ni za uongo kwa kuwa Apple haijatangaza popote kuwa inaendesha zoezi hilo.
Nukta Fakti imepitia tovuti za kampuni ya Apple Inc sambamba na mitandao yake yote ya kijamii inayomiliki, hakuna taarifa zozote za ugawaji wa simu hizo za Iphone.
Pia Apple haina uhusiano wowote na akaunti ya Iphone Giveaway 2020 ambayo ilifunguliwa Julai 4 na kuchapisha taarifa hiyo ya ugawaji wa simu hizo.
Latest