Fahamu undani wa kusajili nembo ya pekee ‘Trade Mark’ Tanzania – 2

September 5, 2020 7:35 am · Hamza Yusuph
Share
Tweet
Copy Link
  • Sheria inatoa nafasi kwa mtu yeyote yule ambaye ana maslahi juu ya usajili wa TM fulani kuwasilisha pingamizi lake mbele ya sheria. 
  • Mmiliki wa nembo ana haki ya kuitumia nembo yake  kwa uhuru bila vikwazo kwa kuzingatia matakwa ya kisheria.
  • Mtu ambaye nembo yake imetumika kinyume na sheria anatakiwa kufungua kesi ili apate ahaki yake. 

Katika makala iliyopita tuliangazia umuhimu wa nembo ya pekee ‘Trade Mark’  na faida zake baada ya usajili kukamilika. Leo tunaendelea kuangazia suala hilo kwa undani kuhusu kuweka pingamizi juu ya usajili wa ™ na ukiukwaji wa nembo za bishara na huduma.


Kuweka pingamizi juu ya usajili wa “Trade Mark”

Sheria inatoa nafasi kwa mtu yeyote yule ambaye ana maslahi juu ya usajili wa TM fulani kuwasilisha pingamizi lake mbele ya sheria. 

Kwa mujibu wa sheria, mtu anaweza kuwasilisha pingamizi lake kuhusu usajili wa TM fulani ndani ya siku 60 tangu tangazo la usajili  kutolewa.

Mleta pingamizi anatakiwa kuwasilisha pingamizi lake kwa msajili wa TM. Mleta pingamizi anatakiwa kuweka bayana sababu ambazo zinamfanya yeye apinge usajili wa TM hiyo. 

Uwasilishaji wa pingamizi umewekwa kisheria kwa kutumia kanuni ya 34 na 35 za Kanuni za Nembo za Biashara na Huduma za mwaka 2002. Pingamizi linapaswa kuwa katika maandishi kwa mleta pingamizi kujaza form nambari TM/SM 34.

Sababu hizo lazima ziwe na mashiko mbele ya sheria, hivyo basi mleta pingamizi anatakiwa kuwasilisha sababu ambazo zitakidhi na kufikia vigezo vya kisheria. 

Kwa mujibu wa sheria sababu hizo zinaweza kuwa kama zifuatavyo:

  1. Usajili unataka kufanywa kwenye huduma au bidhaa ambayo iko kinyume na sheria au maadili. Kwa mfano usajili wa bangi au ukahaba.
  2. Usajili unataka kufanywa kwa sababau kuna TM ambayo tayari imeshasajiliwa kwenye huduma au bidhaa sawa na hiyo au inayoendana na hiyo.
  3. Ikiwa usajili huo utafanyika kwa TM ambayo tayari imesajiliwa  ina hatari ya kudanganya au kupotosha umma.


Sheria inatoa nafasi kwa mtu yeyote yule ambaye ana maslahi juu ya usajili wa TM fulani kuwasilisha pingamizi lake mbele ya sheria. Picha| Legal Desire. 

Ipi haki ya mtu aliyewekewa pingamizi?

Sheria inamtaka msajili kumpelekea aliyewekewa pingamizi nakala  juu ya sababu za pimgamizi na hoja zilizo mbele yake. Mleta maombi anatakiwa kujibu pingamizi kwa kutumia kiapo kinzani na kuwasilisha mbele ya msajili. 

Mleta maombi anatakiwa kuwasilisha kiapo kinzani ndani ya siku 60 kwa mujibu wa kanuni ya 36 ya Kanuni za Nembo za Biashara na Huduma za mwaka 2002. Kiapo kinzanii kinapaswa kuwasilishwa kwa kujaza fomu nambari TM/SM 6.


Usikilizwaji wa pingamizi

Baada ya kupokea hoja zote mbili, msajili wa TM atawasikiliza pande zote mbili mithili ya hakimu anavyofanya katika kesi za kawaida kabla ya kutoa uamuzi juu ya shauri husika. 

Pande zote mbili zitapewa muda wa kuthibitisha na kupinga hoja. Baada ya usikilizwaji huo, Msajili wa TM atatoa uamuzi juu ya pingamizi lililowekwa.

Mtu yoyote ambaye hataridhika na uamuzi wa Msajili atawasilisha rufaa yake mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha Sheria ya Nembo za biashara na huduma ya mwaka 2002.


Soma zaidi:



Ukiukaji wa nembo za biashara na huduma

Mmiliki wa nembo ana haki ya kuitumia nembo yake  kwa uhuru bila vikwazo kwa kuzingatia matakwa ya kisheria. Kwa mujibu wa sheria mmiliki wa nembo anakua na haki zote za kuitumia nembo hiyo kwa muda wote ambao itakua imesajiliwa kisheria.

Swali la msingi ukiukaji unatokeaje?  Unatokea pale ambapo mtu mwingine ambaye hajasajili nembo hiyo anapoanza kutumia nembo hiyo kwenye biashara au huduma zake.

Kwa lugha rahisi ni kwamba matumizi ya nembo hiyo yanaweza kuhatarisha au kupotosha umma juu ya kile kinachoonekana kufanana na nembo halali ambayo imesajiliwa kisheria na inayomilikiwa kisheria. 

Ili kuwe na ukiukaji inaamnisha kuwa kuna nembo ambayo tayari imeshasajailiwa na inatumika kwenye huduma au bidhaa fulani na kuna mtu mwingine ambaye anatumia nembo hiyo kinyume na yule mmiliki halali wa nembo hiyo.


Mdai kwenye shauri la ukiukaji wa nembo anatakiwa kufanya nini?

Mtu ambaye nembo yake imetumika kinyume na sheria anatakiwa kufungua kesi ya madai mbele ya mahakama zetu tukufu kwa mujibu wa sheria. Mdai atakua na kazi nzito mbele ya mahakama kuthibitisha kuwa mdaiwa ametumia nembo yake iliyosajiliwa isivyo halali.

Mdai anatakiwa kuthibitisha kuwa:

  1. Mdaiwa ametumia nembo yake ambayo inasasabisha usumbufu au inachanganya watumiaji au walaji juu ya bidhaa au huduma zake.
  2. Mdaiwa amesababisha au ameuadaa umma kwa namna moja au nyingine kutokana na matumizi ya nembo hiyo.

Mdai atakua katika nafasi nzuri sana ya kushinda madai kama ataweza kuthibitisha haya malalamiko yake mbele ya mahakama tukufu.

Hamza Yusufu Lule ni Wakili wa Mahakama kuu na Mahakama za chini. Kwa msaada wa kisheria wasiliana nami kupitiaTwiter@Hamzaalbhani. Simu: 0717521700.

/
No matches found for this filter
30 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV