Nape: Tumepanua uhuru wa vyombo vya habari Tanzania

May 2, 2022 7:58 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani amepanua uhuru wa vyombo vya habari Tanzania, jambo linalotoa fursa kwa waandishi kutekeleza majukumu yao kwa kujiamini.

Kuelekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mei 3, 2022, Waziri Nape amesema wataitumia siku hiyo kufanya tathmini ya hatua zilizopigwa katika kuongeza uhuru wa kujieleza nchini hasa unahusu vyombo vya habari.

Enable Notifications OK No thanks