Biography

Nuzulack Daunsen
Data analyst
emailnuzulackd702@gmail.com
phone+255 764 176 793
worldhttp://nukta.co.tz/bio/nuzulack
Nuzulack Dausen ni Mwanzilishi Mwenza na Mhariri Mkuu wa kampuni ya Nukta Africa Limited aliyehitimu Shahada ya Sayansi ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Kabla ya kujiunga na Nukta Africa, Dausen aliwahi kushika nafasi mbalimbali katika kampuni ya Mwananchi Communications Ltd inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti ikiwemo ya Mhariri mwanzilishi wa Habari za Takwimu (Data Editor). Amepata mafunzo mbalimbali ya Uanahabari yakiwemo ya Uandishi wa Data (Data Journalism) kutoka Shule ya Uandishi wa Takwimu (Dat Journalism Academy ya Afrika Kusini). Dausen ameripoti matukio mbalimbali makubwa ya kitaifa na kimataifa kama Uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 2016. Uanahabari umemfanya ashinde tuzo mbalimbali za uandishi wa habari zikiwemo za Mwandishi Bora wa Habari za Takwimu Tanzania mwaka 2017 inayotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na tuzo ya Mwandishi Bora Afrika wa masuala ya Nishati na Miundombinu wa mwaka 2017 katika tuzo za Umahiri wa Habari za Zimeo ambazo hutolewa na Taasisi ya African Media Initiative (AMI). Dausen amejikita zaidi katika habari za biashara, uchumi, teknolojia na data.