Biography

Zahara Tunda
Mwandishi wa Teknolojia na Masuala ya Jamii
emailztunda@nukta.co.tz
phone
worldnukta.co.tz
Zahara Tunda ni mwandishi wa habari aliyejikita katika uandishi wa masuala ya Kijamii, Teknolojia, na Data (Takwimu). Amehitimu Shahada ya Mawasiliano kwa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Zahara amepata tuzo mbalimbali za uandishi ikiwemo ya Mshindi wa Tuzo za Mashindano ya Uandishi wa Hadithi Fupi za Andika na Soma mwaka 2014/2015. Pia, amepata mafunzo mbalimbali ya uandishi ya habari ikiwemo mafunzo ya miezi sita ya uandishi wa habari za Usalama Barabarani yaliyofadhiliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2017. Kwa sasa ni mwandishi wa habari wa kampuni ya Nukta Africa Limited.