Wanafunzi 131,986 wachaguliwa kujiunga na kidato cha tano 2024

May 30, 2024 2:17 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Kati yao 6,576 wamepangiwa shule za kutwa na wengine 123,948 shule za bweni.
  • Wanafunzi 1,462 wapanguwa shule za vipaji maalum.

Dar es Salaam.  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa ametangaza orodha ya watahiniwa 188,787 waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano kwa shule za Serikali na vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi mwaka 2024.

Kati ya hao, wanafunzi 131,986  sawa na asilimia 69.9 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kidato cha tano 622 zikiwemo shule mpya 82 zinazoanza mwaka huu wa 2024 ambapo ni wasichana ni 66,432 na wavulana ni  65,554.


Soma zaidi:Orodha ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano 2024 hii hapa


Waziri Mchengerwa aliyekuwa akizungumza na wanahabari leo Mei 30, 2024 amesema kuwa wanafunzi 1,462 kati ya wanafunzi hao wamefaulu vizuri zaidi na kupangiwa kujiunga na shule maalum.

“Wanafunzi 1,462 wakiwamo wasichana 669 na wavulana 793 walipangwa katika shule za sekondari nane zinazopokea wanafunzi wenye ufaulu wa juu zaidi ambazo ni Kilakala, Mzumbe, Ilboru, Kisimiri, Msalato, Kibaha, Tabora Boys na Tabora Girls,” amesema Mchengerwa.

Aidha Mchengerwa amebainisha kuwa  wanafunzi 6,576 wakiwamo wasichana 3,449 na wavulana 3,127 wamepangwa katika shule za sekondari za kutwa za kidato cha tano.

Wanafunzi wengine 123,948 wakiwemo wasichana 62,636 na wavulana 61,312 wamepangiwa katika shule za sekondari za bweni za kitaifa za kidato cha tano.

Miongoni mwa wanafunzi hao watakaojiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya kati katika mwaka wa masomo 2024/2025 812wana mahitaji maalum.

Enable Notifications OK No thanks