Air Tanzania yapokea ndege ya mizigo kupunguza maumivu kwa wafanyabiashara

June 3, 2023 2:08 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Inategemewa itaimarisha shirika la ndege Tanzania (ATCL) na kuwa mkombozi kwa wakulima na wafanyabiashara
  • Sasa ATCL kuwa na ndege 13, ikikusudia kufikisha 20 mwaka 2027
  • Ombi la ndege nyingine ya mizigo kufanyiwa kazi na Rais Samia

Dar es Salaam. Hatimaye Tanzania imepokea ndege ya kwanza ya mizigo, hatua itakayoisaidia kukuza Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) na kuleta unafuu kwa wakulima na wafanyabiashara wanaoagiza au kuingiza mizigo nje ya nchi. 

Ndege hiyo aina ya Boeing 767-300F iliwasiri katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam ikipokelewa na mamia ya watu wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan. 

Ujio wa ndege hiyo, yenye uwezo wa kubeba tani 54 za mizigo, unafanya ATCL kuwa na ndege 13 zikiwemo ndege mbili za Boeing 787 Dreamliners, ongezeko la kasi tangu Serikali ianze mikakati ya kulifufua miaka saba iliyopita.

Ujio wa ndege hiyo, yenye uwezo wa kubeba tani 54 za mizigo, unafanya ATCL kuwa na ndege 13 zikiwemo ndege mbili za Boeing 787 Dreamliners, ongezeko la kasi tangu Serikali ianze mikakati ya kulifufua miaka saba iliyopita. 

Tani 24,521 za maua, mbogamboga, nyama na samaki zilisafirishwa kwenda katika masoko ya kimataifa mwaka uliopita kwa kutumia ndege za mashirika ya nchi jirani na kuongeza gharama za usafiri kwa kuwa ndege za ATCL zilimudu kusafirisha tani 420 tu.

Mkurugenzi wa ATCL Ladislaus Matindi, aliyekuwa akizungumza katika hafla ya kuipokea ndege hiyo leo (Juni 3, 2023), amesema usafirishaji mazao hayo kwa kutumia nchi za jirani sio tu kuliongeza gharama bali hupunguza thamani ya mazao hayo kutokana na kukaa muda mrefu.

Matindi ameongeza kuwa mpango mkakati wa shirika hilo ni kuwa na ndege 20 ifikapo mwaka 2027 ambapo kati ya hizo ndege nane ni za masafa mafupi, nane za masafa ya kati, tatu za masafa marefu pamoja na ndege moja ya mizigo.

Kwa sasa ndege nyingine tatu zinaendelea kuundwa ikiwemo Boeing  787-8 inayotarajiwa kupokelewa Tanzania mwaka huu. 

ATCL ni miongoni mwa mashirika ya umma ambayo yamekuwa yakiripoti hasara katika uendeshaji wake ndani ya miaka 10 iliyopita. 

Hata hivyo, Matindi amesema wamekuwa wakipunguza hasara mwaka hadi mwaka kutokana na kuimarika katika uendeshaji wake. 

Amesema hasara imepungua takriban mara tatu ndani ya miaka sita kutoka Sh110 bilioni mwaka 2015/16 hadi Sh35.2 bilioni mwaka 2021/22.


Soma zaidi


Miongoni mwa changamoto ambazo zimekuwa zikilikabili shirika hilo na kusababisha kupata hasara ni pamoja na gharama kubwa za uendeshaji zisizo za kioparesheni, madeni, ndege kutofanyiwa matengenezo kwa wakati pamoja na uchache wa watumishi katika kada ya urubani na uhandisi.

Rais Samia kufanyia ombi la ndege nyingine ya mizigo 

Ili kuimarisha utendaji kazi wa ATCL katika sekta ya usafirishaji wa mizigo Matindi amemuomba Rais Samia kuongeza ndege nyingine ya mizigo, ombi ambalo mkuu wa nchi ameahidi kulifanyia kazi ombi hilo.

Katika moja ya hotuba fupi alizowahi kuzitoa iliyochukua chini ya dakika tatu, Rais Samia amewashukuru Watanzania kuwaombea kufanya mambo ya maendeleo. 

“Mtuombee tufanye kazi tupate mapato tuweze kuendelea na mambo kadhaa, kumeombwa ndege nyingine ya mizigo, ahadi yangu kwenu wananchi ni tunaifanyia kazi,” amesema Rais samia kabla ya kwenda kuikagua ndege hiyo.

Enable Notifications OK No thanks