Rais Samia kufanya ziara Afrika kusini kushuhudia uapisho wa Ramaphosa

June 18, 2024 2:12 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni ziara ya kikazi ya siku moja
  • Uapisho kufanyika Juni 19, 2024

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kuondoka nchini jioni ya leo Jumanne Juni 18, 2024 kwenda Afrika Kusini kwa ziara ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya kushiriki hafla ya uapisho wa Rais Mteule, wa taifa hilo Cyril Ramaphosa.

Taarifa iliyotolewa na Sharifa Nyanga, ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu imebainisha kuwa Rais Samia atashiriki hafla hiyo itakayofanyika kesho Jumatano Juni 19, 2024 baada ya Ramaphosa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa nchi hiyo.

Ramaphosa alichaguliwa tena kuwa Rais wa Afrika Kusini na Bunge la nchi hiyo Ijumaa ya Juni 14, 2024 kufuatia makubaliano kati ya chama tawala cha African National Congress (ANC) na vyama vya upinzani mara baada ya kushindwa kupata zaidi ya asilimia 51 ya kura inayohitajika ili kuunda Serikali.

Enable Notifications OK No thanks