Mbinu za kupata picha kali kwa kutumia kamera ya simu yako

January 8, 2022 8:07 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kufuta lenzi ya kamera yako kabla ya kupiga picha.
  • Tumia misttari ya “grid” kupata picha kali zaidi.
  • Zingatia mwanga kwa fanani wako.

Dar es Salaam. Kuwa na simu janja yenye kamera nzuri ni jambo moja lakini kupata picha nzuri kwa kutumia simu hiyo ni jambo lingine. Kama unabisha, chukua simu ya mjomba wako kisha tazama selfie (picha za kujipiga) zake. Natania tu.

Inahitaji maujanja fulani hivi na mbinu za kuitumia ili kila picha unayoipiga, watu waulize aina ya simu unayoitumia.

Kupata picha nzuri, ni kweli utahitaji simu ambayo kamera yake inaeleweka. Tovuti ya masuala ya upigaji picha kwa simu, The Smartphone Photographer imeandika kuwa, kamera yenye “megapixel” (MP) 12 na kuendelea.

“Kama utauza picha zako au kutengeneza machapisho makubwa, simu yeye kamera yenye MP12 au 16 au zaidi itafanya kazi nzuri,” imeandika tovuti hiyo.

Ili upate picha poa, unatakiwa kujifunza kutumia mistari ya gridi kupiga picha ambayo itakusaidia kupata picha za wima na zinazoonyesha ulichodhamiria kuonyesha kwenye picha.

Pamoja na hayo, inashauriwa kuseti “focus” ya picha yako kwa kubonyeza skrini yako katika eneo la unachokipiga picha. Pia hakikisha kioo cha kamera yako ni kisafi ili kupata picha maridhawa.

Zaidi, tazama hii kujifunza

                         

Enable Notifications OK No thanks